Pages

Sample Text

Frank Kimaro run this blog

10/05/2011

Baadhi ya mambo yanayotokea katika mpaka wa Tanzania na Kenya maeneo ya Himo mkoani Kilimanjaro.

                                           Baadhi ya bidhaa zilizozuiliwa na T.R.A kwa ajili ya
                                                    ukaguzi zaidi hii inaonesha ni jinsi gani
                                          uvushaji wa bidhaa za magendo kwenye mpaka huo.
                                      Haya ni magari ambayo hutumika kusafirisha mizigo kwenye 
                                     mpaka huu wa Tanzania na Kenya lakini mara nyingi hufanya
                                 kazi  hiyo usiku sasa swali la kujiuliza ni hili Kwa nini bidhaa nyingi
                                          zinasafirishwa usiku na sio mchana?

 Hapa ni katika ardhi ya Kenya na ndiyo sehemu inayokagua
watu wanaoingia na kutoka nchini Kenya lakini cha ajabu waendesha 
pikipiki maarufu kama bodaboda wao hupita bure Je katika kupita
kwao hawawezi kuvusha bidhaa kinyume na taratibu zilzowekwa?  
                             Bado naendelea na safari yangu nikiwa nchini Kenya nikagundua hili lifuatalo,
                                          Nikagundua kuna njia iliyobuniwa na waendesha pikipiki
                                           kwa ajili ya kuvusha magendo kutoka nchini kenya kama
                                                            inavyoonekana pichani hapo juu.



                              Kama unavyoona pichani pikipiki ndo usafiri mkubwa katika maeneo
                                                                         ya mpakani.
                                  Tunapaswa kutambua kuwa uvushaji wa magendo ni hatari kwako na kwa
                                                        taifa kiujumla.