MITAA INAVYOSEMA KUHUSU CHANZO CHA KIFO:
MWIGIZAJI nguli Tanzania, Steven Kanumba amefariki dunia ghafla nyumbani kwake maeneo ya Sinza Vatican, Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo.
Chanzo kimesema kuwa Kanumba alifariki wakati akiwa anagombana na mpenzi wake, mwigizaji mwenzake, Lulu.
“Alikuwa anagombana na Lulu. Lulu akamsukuma Kanumba, akaangukia kichwa, ndio akafa, ilikuwa saa tisa usiku,”kilisema chanzo.
bongostaz inaelekea eneo la tukio ambako inaelezwa tayari mamia ya watu wamekwishafika ili kukupasha habari zaidi.