Pages

Sample Text

Frank Kimaro run this blog

11/04/2011

Uchunguzi binafsi uliofanywa juu ya Dk. Harrison Mwakyembe

Hatua ya kwanza:

Mchunguzi aliamua kujua kama ni kweli kalishwa sumu au laa. Na watu alio wahusisha katika kujua huko ni
TISS.

Katika uchunguzi aliweza kuzungumza na LTK wapatao kumi na tano. Maboharia wawili,Wapanga mikakati wawili Mkuu wa LTK,Vijana wa kazi kumi,Wote maelezo yao yalifanana kwa maana ya (walishiriki kupanga na kutekeleza kumlisha sumu Dr Harison Mwakyembe)

Hatua walizopitia:

Kwa mujibu wa maelezo ya LTK/D00/B1 mkuu wa kitengo hicho ambae kwa kweli aliongea nae kama rafiki yake wa karibu ndie aliyempa mwangaza wakufanikisha kazi yake.

Katika misheni hii watu wengi wanatakiwa KUFA, akawataja wale muhimu tu:
1. Wilblod Slaa
2. Samweli Sitta
3. Harison Mwakyembe
4. Said Kubenea
5. Mark Mwandosya
Mnamo ijumaa ya tarehe 01/10/2010 saa 4:25, kikao kikuu cha mikakati kilikalika Moven Pick kikihudhuriwa na watu sita,


TISS/A001 XXX

TISS/B1

TISSB32

TISS/B5

TISS/A6

TISS/F5
Baada ya mjadala wa saa moja uliogusa magumu inayokumbana serikali na watu walio waona wao ni vikwazo na waliosababisha magumu hayo, ndipo wakaibuka na listi ya wanaotakiwa kusalimisha uhai wao:

Bada ya hapo kesho yake TISS/B1 alikutana na LTK/D00/B1 na kumpa amri ya misheni hiyo na orodha kamili ya watuhumiwa bila kumwambia sababu za mauaji hayo, zaidi alisema “nahitaji ripoti ya utekelezaji”.

Baada ya amri kuwa chini ya LTK, mikakati ya aina ya kifo kwa kila mtuhumiwa ilipangwa ambapo walipamgwa katika makundi matatu,

1 Samweli Sitta
2 Harison Mwakyembe
3 Mark Mwandosya
Hawa wamepangiwa vifo vya aina mbili kwanza ajali na ikishindikana watalishwa sumu.

1 Said Kubenea

Kumwagiwa tindikali, baada ya kufeli ile ya kwanza imeagizwa nyingine toka Bulgaria yenye kuua baada ya masaa kumi na mbili tu!

1.Wilblod Slaa

Huyu anatakiwa kufa kwa shabaha ya risasi (snipers) ndio wanao andaliwa tu kwa sasa.

Waliopewa kipaumbele kufa ni Samweli Sita, Mark Mwandosya na Harison Mwakyembe ambapo LTK/D00/B10, LTK/D00/B14, LTK/D00/B17 na LTK/D00/B21 walipewa kazi hiyo.

Kikwazo kikuu walichokumbana nacho vijana wa kazi, ni kuwa, Sita, Mwandosya na Mwakyembe wote ni majasusi na kwapamoja walifanikiwa kufumbua njama hizo chafu za mauaji kwa siri.

Mitego ya ajari 16 kwa Mwakyembe yote imemkosa, 12 kwa Sita nayo ikamkosa,7 kwa Mwandosya nae kakoswa.

Walipoona mbinu zote za vifo vya ajali zimefeli wakahamia kwenye aina ya pili ya vifo vya kulishwa sumu:

Katika aina hii ya mauaji kwa muujibu wa vijana wa kazi wanashangaa uimara wa Samweli Sita na Mwakyembe kwani wameshalishwa aina nyingi za sumu lakini bado wanadunda tu, kwanza sumu ya kwanza kuwalisha ni katika kikao cha kwanza cha bunge mwa 2011, hawakupata madhara yoyote.

Wakabadilishiwa aina ya sumu, hakika hii ilimpata zaidi Mwandosya kwani ilipandikizwa katka simu yake ya mkononi bila yeye kujua saa 4:40 asubuhi ofisini kwake tarehe 7/3/2011.

Aina hii ya sumu (jina sikupata kujua lakini hapa huitwa LTK/XXX) nayo ilishindwa kuzaa matunda kwa Mwakyembe na Sita licha ya kupewa katika mazingira tofauti,hii ilitokana na kuwa kidogo.


Zoezi hili zito na la hatari baada ya kuwa gumu kupita kiwango kwa kuwa hata Mwandosya hakudhurika sana, ilibidi uhitajike msaada toka nje ya nchi na ndipo jasusi mashuhuri wa kitanzania Exaveri H.Limo akaenda Urusi kutafuta aina nyingine ya sumu kali.

Tarehe 11/7/2011 akafanikiwa kukutana na Zudrav Ghev mmoja wa wakemia wa KGB katka kituo cha Moscow akapata Polonium 236, kutokana na unyeti na hatari ya sumu hiyo ilimlazimu bwana Zudrav Ghev kuchukua ndege ya watu wa tano na kuruka mpaka tz .

Baada ya kufika tz bwana Zudrav alitoa mafunzo ya wiki moja jinzi ya kuhifadhi na kutumia kisha akatokomea kurudi kwao na vijana wake wanne.

Baada ya Mrusi kuondoka misheni zikaendelea na mnamo tarehe 24 /7/ 2011 wakati afya ya Mwandosya ikiendelea kuzorota mmoja wa LTK/D00/B10 wa kike alifanikiwa kumuwekea Polonium 236 katika chai nyumbani kwake akiwa ni miongoni mwa watu waliokwenda kumjulia hali,

Na Mwakyembe alikuja kuwekewa ktk maji ya kunywa na kwenye kitambaa cha kufutia uso LTK/D00/B17 siku ya uzinduzi wa kikao cha Makandarasi,Wahandisi na Wakadiriaji majenzi pale Mlimani City kilichohudhuriwa na rais.

Kuonyesha kuwa Mwakyembe ni jasusi aliye kubuhu siku hiyo maji hakuyanywa wala kugusa kabisa lakini mungu si athumani kitambaa akakitumia, jambo la kushangaza nikuwa baada ya kama dakika 20 kukitumia kile kitambaa alikitupa wakati anatoka eneo la Mlimani City.

Hivi sasa LTK wameshamaliza kazi yao kwa watu wawili na anayefuata ni Samweli Sita
Na uwezekano wa kupona kwa India ni mdogo ila wanaweza kupunguza makali na kusogeza mbeli mauti yao hiyo ni kwa mujibu wa mkuu wa LTK.

Slaa maandalizi yake yanaangalia zaidi uchaguzi ujao ingawa kumeingia aina ya mabishano makali juu ya kumuua hasa wakihofia kutokea kwa vita ya wenyewe kwa wenyewe kwakuwa jamii ya kitanzania na kimatafa inamtambua.

Said Kubenea amekabidhiwa LTK/D00/B21 ambae anasubiri kitendea kazi toka Bulgaria ambapo jasusi Yugrov Dittzov ndie atakae ileta.Huu ndio uchunguzi wake binafsi baada ya kupata taarifa juu ya hali ya Dr Harison Mwakyembe kuwa ni tete.

anaongezea kusema kuwa serikali ya Tanzania inafanya mauaji ya raia wake hasa viongozi wenye mtazamo tofauti na serikali.Mwisho anaiomba serikali ya Mh rais isikilize kilio cha watanzania isisikilize kilio cha wa kwasi na mafisadi.

Kwa msisitizo anawaomba watanzania tuungane pamoja bila kujali dini zetu,makabila yetu wala rangi zetu kulikataa kundi hili la wahalifu lisilozidi watu 30.

Huu ni uchunguzi wake, unayohaki ya kusubiri uchunguzi wa madaktari wa India

11/02/2011

Zitto Kabwe alivyowaandikia watanzania juu ya hali yake.

   
Ndugu zangu,

Kwanza kabisa napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa kuniwezesha muda huu kuwa na nguvu za kukaa katika kiti na kuweza kuandika haya machache kwenu. Nawashukuru sana Wanamabadiliko kwa salaam zenu nyingi za pole mara mliposikia ninaumwa na kulazwa hospitalini. Najua hamkuwa na taarifa kamili za kuumwa kwangu na kwa kweli suala la kuumwa ni suala la mtu binafsi (hata kwa mtu mwenye dhamana ya kiuongozi wa umma japo umma nao una haki ya kujua kinachomsibu kiongozi husika).
Mwanzo
Nilianza kupatwa na maumivu ya kichwa usiku wa siku ya Ijumaa tarehe 20 jijini Dar es Salaam mara baada ya kuwasili kutoka Jimboni tayari kwa kazi za Kamati za Bunge ambapo Kamati yangu ilikuwa imekwishaanza kazi wiki hiyo kwa kupitia mahesabu na utendaji wa Mamlaka za Maji nchini.
Kama kawaida yangu niliona maumivu hayo makali kama ni sehemu tu ya uchovu wa ziara za Jimboni na safari za mara kwa mara nilizofanya kuinigilia ziara za Jimboni ikiwemo kuhudhuria Mdahalo wa Umeme na Mkutano wa Uwekezaji Kanda ya Ziwa Tanganyika.
Hivyo nililala na nilipoamka kichwa kilikuwa kimepona na hivyo nikahudhuria kikao cha Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma katika Ofisi ya Bunge mpaka saa saba mchana.
Siku ya Jumapili saa kumi na moja jioni nikiwa katika Hoteli ya Southernsun nilipatwa na homa kali ghafla. Nilikatisha mkutano niliokuwa nao na kuamua kurejea nyumbani, lakini nilishindwa kuendesha gari na hivyo kumwomba Dereva wa Mhe. Mhonga anifuate ili anisadie kunifikisha nyumbani.
Nilipofika nyumbani kwangu Tabata, homa ilizidi kupanda na hivyo kuamua kwenda Hospitali mara moja. Nikapelekwa Agakhan Hospital na nikapata huduma.
Nilipochukuliwa vipimo ilionekana sina malaria wala homa ya matumbo na pia hawakuweza kuona sababu ya homa ile namna ile (maana ilifikia degree 40).
Walituliza homa, nikapewa Panadol na baadaye nikaruhusiwa kurudi nyumbani mnamo saa tano usiku. Nilipoamka siku ya Jumatatu nikaenda kazini kuongoza Kikao cha Kamati ya Bunge ambapo tulikuwa tunashughulikia Hesabu za Bodi ya Utalii na Benki ya Posta Tanzania.
Nilipita Agakhan kupata majibu ya ziada na kuambiwa nipo sawa ila nipumzike nisifanye kazi kwa siku kadhaa na nitakuwa sawa.
Hali kubadilika
Siku ya Jumanne niliamka nikiwa salama, kichwa kikiuma kwa mbali lakini sio vya kutisha. Nikawajulisha wajumbe wenzangu wa kamati kuwa sitakwenda kazini na wao waendelee na kazi.
Hata hivyo ilipofika saa sita kamili nilianza kutetemeka mwili mzima na homa kuwa kali sana huku kichwa kikiniuma sana sana sana!
Dada zangu wakamwita Driver na kunikimbiza Hospitali ya Agakhan. Wakarejea vipimo vilevile na matokeo yakawa yaleyale. Joto lilifika degree 39.8 Hivyo wakanipa dawa za kupoza homa na maumivu ya kichwa kwa drips na sindano kadhaa.
Siku ya pili hospitalini nikafanya vipimo zaidi ikiwemo ultra sound na vyote kuonekana sina tatizo lolote. Niliendelea kuwepo Hospitali na kwa kweli hali ilikuwa inatia moyo sana kwani nilipata nguvu na hata kuweza kuzungumza, homa ilikuwa imepungua sana.
Pamoja na kwamba Mganga Mkuu wa Serikali kwa kushirikiana na Waziri wa Masuala ya Bunge na Daktari wangu binafsi kuwataka waangalie upya vipimo vya malaria, madaktari wa Agakhan waliwahakikishia viongozi hawa na Daktari wangu kwamba hawajaona Malaria na hivyo wanaendelea na uchunguzi wa ‘a trigger’ ya homa kali niliyokuwa napata.
Hali kuwa Mbaya
Usiku wa siku ya Jumatano Hali ilikuwa mbaya sana. Joto lilipanda tena kufikia 40 na kichwa kuuma zaidi. Nilikuwa kama ninatwangwa kwenye kinu kwa kweli. Nilikuwa natetemeka sana. Ilikuwa taharuki kubwa sana katika chumba nilicholazwa.
Wageni waliokuwa wamekuja kunijulia hali wakati hali inabadilika ilikuwa ni pamoja na Ndugu Murtaza Mangungu na Mohamad Chombo ambao ni wajumbe wa Kamati ya Bunge ya POAC, walishauri mara moja nihamishwe Hospitali kupelekwa Muhimbili.
Muda si mrefu kupita Waziri Lukuvi na Katibu wa Bunge walifika, wakaafiki na nikahamishiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili na kwa hali niliyokuwa nayo nikalazwa katika Chumba wanachokiita Mini-ICU. Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Mama Blandina Nyoni alikuwepo Hospitalini tayari.
Usiku huo huo nilifanyiwa vipimo upya. Full Blood picture pamoja na BS. Vile vile kufuatia malalamiko kuhusu maumivu ya kichwa ikaamuliwa kuwa nifanyiwe CT Scan usiku ule.
Ikaonekana nina wadudu wa Malaria 150 na mara moja nikaanza matibabu. Namshukuru sana Daktari kijana Dkt. Juma Mfinanga kwa umahiri mkubwa aliouonyesha tangu nilipofika pale Mini ICU.
Asubuhi ya siku ya pili nikapata majibu ya tatizo la maumivu ya kichwa. Nimekuwa nasumbuliwa na kichwa kwa miaka zaidi ya Kumi sasa na katika kipindi hicho mara nne nilipoteza fahamu na kuanguka (Mara ya kwanza mwaka 2000 nikiwa Jijini Mwanza nikielekea kwenye Mkutano wa Vijana wa National Youth Forum, Mara Pili Mjini Dodoma katika mkutano kama huo mwaka 2001 lakini ilikuwa usiku, Mara ya tatu Nikiwa chumbani, Hall II mara baada ya kutoka *Prep, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 2002 na mara ya Nne Bungeni siku ya kupitisha Muswada wa Madini 2010 kufuatia wiki nzima ya Kamati na Mjadala wa Bunge (Ndugu Katulanda anakumbuka siku hii kwani yeye ndiye niliyemkamata njiani kunikimbiza Zahanati ya Bunge).
Tatizo lililogundulika ni SINUSITIS, ambayo tayari imekuwa sugu. Daktari Bingwa wa magonjwa haya Dkt. Kimaryo akanieleza kwa kirefu juu ya tatizo hili na kuniambia suluhisho ni ‘surgery’ na pale Hospitali ya Taifa hawafanyi hiyo operesheni. Akashauri niletwe India ambapo kuna Daktari mpasuaji wa ugonjwa huu. Nikakubali.
Baada ya kuwa Malaria imedhibitiwa kwa kufikia nusu ya ‘dozi’ nilopewa na wadudu kuonekana kutokomea, Ofisi ya Bunge ikaandaa safari. Nimefika India. Nimebakiza sindano mbili ili kumaliza ‘dozi’ hiyo na tayari nimefanyiwa taratibu zote kwa ajili ya ‘surgery’ hiyo.
Sijafa
Uvumi ulienezwa nimekufa. Kwa kupitia kwenu ndugu zangu Wanamabadiliko, napenda Watanzania wenzangu wajue mimi ni mzima wa Afya. Nimepata maradhi kama Binadamu mwingine yeyote anavyoweza kupata na namshukuru Mungu kwamba ninapata matibabu mazuri kabisa.
Shukran
Nawashukuru sana Madaktari wa Hospitali ya Taifa Muhimbili chini ya Prof, Mwafongo kwa juhudi kubwa walioonyesha katika kunihudumia. Naishukuru Ofisi ya Bunge kwa Kutimiza wajibu wao kwangu kama Mbunge, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya kwa kuonyesha upendo wa hali ya juu na watumishi wote wa Wizara ya Afya, Katibu Mkuu wa CHADEMA Dkt. Slaa kwa ufuatiliaji wa karibu wa Afya ya Naibu wake, Wabunge wajumbe wa Kamati ya POAC, Dkt. Alex Kitumo, ndugu, jamaa na marafiki zangu wote.
Nawapa pole wananchi wa Jimbo la Kigoma Kaskazini kwa uvumilivu mkubwa hasa kufuatia uvumi mbalimbali ulioenezwa, pia Watanzania wengine kwa uzito huo huo.
Nitawajulisha kwa lolote Mungu akipenda. Ninaendelea na matibabu na hali yangu ni nzuri
Ndugu yenu
Zitto

Na huu ndio waraka wa Godibless Lema kwa wananchi wa Arusha na Tanzania kwa ujumla.

WAARUSHA NA WATANZANIA WAPENDA
MABADILIKO KOKOTE KULE WALIPO ULIMWENGUNI
JELA NI MAHALI PA KUISHI KAMA SABABU YA KWENDA HUKO NI VITA DHIDI YA
UONEVU, UKANDAMIZAJI WA HAKI NA UTU WA BINADAMU.



Wapendwa wapiga kura wangu na Watanzania wenzangu.
Sina wakati mgumu kuchukua maamuzi haya yanayotokea leo. Upendo huu nilio nao kwa watu wa Arusha na nchi yangu ni sababu ya msingi ya maamuzi haya. Nimetishwa mara nyingi, rafiki zangu wametishwa, jamii ya watu duni imeendelea kuishi kwa mashaka na matisho kwa muda mrefu.
Katika mazingira haya, nikawaza sana kuwa anatakiwa kutokea mtu mmoja jasiri atakayeweza kuona thamani ya watu wengine. Huyo mtu anaweza kuwa wewe lakini kwa wakati huu siwezi kumsubiri tena na nimechagua kuwa mimi nikiamini kuwa utanikuta nikiendelea na safari ya ukombozi.
Tupo wengi sana tunaotaka mabadiliko, haki na ukweli. Hata hivyo hofu, woga na mashaka yamepoteza thamani yetu yote ya maana ya kuishi.
Waliofungwa kwa kuonewa na kuteswa, waliokosa chakula na kulala nje, waliokwenda hospitali na kukosa madawa, waliokosa ajira na kipato mpaka kujikuta wametoroka familia zao, waliopoteza matumaini ya maisha, waliopora utajiri wa nchi yetu kwa manufaa yao binafsi, walionunua haki na sheria dhidi ya wajane na wanyonge na kuwapora vipato vyao vidogo na mashamba yao, USIULIZE SABABU NINI!
Nimetafakari sana na nikatambua kuwa sababu ni mimi pale nilipokuwa kimya wakati wajane na wanyonge wanaonewa.
NIliposikia wengine wanaandamana kupinga uovu, uonevu, wizi, ufisadi na ukandamizaji wa haki nikasema ni hao na wala sio mimi, kumbe nilipaswa kuwa mbele katika harakati hizi.
Nilipoona wenzangu hawawezi kupata matibabu nikasema mimi sio mgonjwa, nilipopata taarifa za rafiki zangu kufungwa kwa makosa yasiyo yao, nilipoona watoto wa mitaani wanaomba chakula, nilipoona wazee wamepoteza matumaini ya kuishi katika uzee wao, nilipoona vijana hawana ajira, nilipoona mabinti wasichana wadogo wameamua kufanya biashara ya ukahaba, NIKATAFAKARI,TENA NIKATAFAKARI, dhahabu zetu, almasi yetu, Milima na mabonde yetu, Tanzaninte yetu, samaki wetu, Uranium yetu, makaa ya mawe yetu, utalii wetu, ardhi na kilimo chetu na zaidi utu na mahusiano yetu.


Na sasa siwezi kukaa kimya tena. NI afadhali vita inayotafuta haki na usawa kuliko amani inayopumbaza na kudhalilisha utu wa mwanadamu. Na katika msingi huu hofu na mashaka vimekosa thamani kwangu, sitamwogopa mtu yoyote, mwenye silaha yoyote, mwenye cheo chochote na wala sitaogopa jela yoyote katika kupigania haki, utu wa kweli katika jamii yangu.


Wanafikiri wataendelea kutuogopesha kwa sababu wana jela na silaha, wanafikiri tutaendelea kuabudu uoga, wanafikiri wataendela kutunyanyasabila sababu ya msingi LAKINI SISI TUNAJUA TUTASHINDA KWA SABABU HAKI TUNAYOIPIGANIA NI MAKUSUDI YA MWENYEZI MUNGU.
Leo nitakwenda jela kwa hiari yangu binafsi kwa siku kadhaa na si kwa NIA YA KUJITAFUTIA UTUKUFU WANGU bali ,” JELA NI MAHALI PA KUISHI KAMA SABABU YA KWENDA HUKO NI VITA DHIDI YA UONEVU, UKANDAMIZAJI WA HAKI NA UTU WA BINADAMU.Kila mara nilipotishiwa nikagundua wanaonitishia, wananitishia kwa jela na mauti. Na mimi nikagundua na nikatambua ni afadhali kuishi miaka hamsini jela huku sababu ikiwa ni kupinga uonevu na ukandamizaji kuliko maisha ya woga na anasa yasiyo na kusudi katika kutetea utu na heshima ya mwanadamu mwenzangu.
Wale mlionitishia kunipeleka jela sasa nimetangulia kwa hiari yangu na wale mliobaki msiogope jela endeleeni kupigania ukombozi utakaoleta usawa katika nchi yenu.
Watakaotubeza na kututukana wasameheni kwani wanahitaji ukombozi wa fikra, watakaotupongeza na kutuonea huruma wafundisheni ujasiri na waambieni mapambano bado yanaendelea tunahitaji umoja wao. Nitarudi mapema. MSIOGOPE, MSIOGOPE, MSIOGOPE , MUNGU YUPO UPANDE WETU.


Mhe Godbless Lema (MB) – Arusha Mjini 31 Oktoba 2011.

11/01/2011

Hali ya Zito kabwe yazidi kuwa mbaya.

Zito Kabwe akia amelazwa hospitalini Muhimbili
(picha kutoka kwenye mtandao)
HALI ya Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) bado ni tete na sasa anapelekwa nchini India kwa matibabu zaidi.
Kwa mujibu wa taarifa ambazo gazeti hili imezipata mchana huu kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili alipokuwa amelazwa, ni kwamba kiongozi huyo ameshauriwa kupelekwa nchini India kwa matibabu zaidi.
Taarifa zaidi zinasema tayari ameelekea katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, na anatarajiwa kuondoka na ndege ya Emirates mchana huu.
“Anapelekwa India kwa matibabu zaidi na huu ni ushauri ambao amepewa na madaktari ambao walikuwa wakimtibu…wanasema anaitaji uangalizi na utulivu wa hali ya juu kimatibabu hivyo wameamua apelekwe nchini India,” alisema kiongozi mmoja wa Chadema akizungumza kwa njia ya simu na mtandao huu.
Mbali na kuzuka kwa taarifa za kutatanisha na za kushtua juu ya hali ya Mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini, jana ililipotiwa kuwa hali yake ni mbaya na amehamishiwa katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU).
Awali Zitto alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Aga Khan, na hali yake ilivyobadilika ghafla jana jioni alipelekwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili. Zitto alilazwa Aga Khan juzi jioni baada ya kusumbuliwa na maumivu ya kichwa kabla ya kuruhusiwa na kisha kurudishwa baada ya maumivu hayo kuendelea.