Pages

Sample Text

Frank Kimaro run this blog

12/17/2011

Mawaziri na wabunge walivyokua kwenye muda wa mapumziko katika kikao cha bajeti



         spika wa bunge la chuo cha Tumaini akiwa anajadiliana jambo na wabunge wakati wa chakula


waziri wa HIV/AIDS akiwa katika pozi
                         Waziri wa katiba na sheria(kushoto) akiwa na naibu spika wa bunge

                           Naibu waziri wa habari (kushoto) akiwa anadoea chakula cha mbunge


                                 Waziri wa makazi akiwa anakula chakula chake taratibu


                                      Naibu waziri wa mikopo naye katika pozi mida ya lunch


                                 Baadhi ya wabunge wakiwa wamejibana sehemu wanakula

                           Waziri mkuu naye mida ya chakula akawakilisha vyema kabisa

                        Mbunge anayewawakilisha wanafunzi wa Journalism akiwa katika pozi

                                     Naibu waziri mwingine wa mikopo akiwa anakunywa maji tu

Mwanamichezo maarufu Shikide akiwa anabugia bila kuogopa kukabwa huku akiwa mmoja wa wanasoka walioalikwa kwenye kikao cha bunge.

Wanamichezo waliolikwa bungeni walipokuwa kwenye lunch

Mawaziri wakiwa wanasubiri kwenda kusoma katiba zao bungeni katika chuo cha Tumaini



Ofisini kwa raisi mambo yalikua hivi



12/16/2011

Andrew Ayew atangazwa kuwa mchezaji bora wa BBC Afrika kwa mwaka huu 2011.

Ayew ametajwa kuwa mchezaji bora wa Afrika huku ikidhihirika wazi kuwa anafuata nyendo za baba yake Abeid "pele" ayew ambaye alishinda tunzo ya BBC mwaka 2011.

Ayew alisema kuwa anaheshimu tuzo hiyo na anashukuru sana kwa watu wa Ghana,Afrika na dunia kwa ujumla ambao walimpigia kura na kusababisha kuipata tuzo hiyo. Ayew au Dede kama anavyofahamika anakuwa ni mchezaji wa tano kutangazwa kama mchezaji bora wa BBC Afrika, wa kwanza alikuwa baba yake akifuatiwa na Sammy Kuffour (2001), Michael Essien (2006) pamoja na Assamoah Gyan(2010).

Afariki baada ya kuchoma sindano ya kuongeza uume



Huko New Jersey,  kijana wa miaka 22 amefariki dunia baada ya kuchomwa sindano ya 'silicone' kwenye ume wake! Eti alitaka iwe kubwa zaidi! Jamani!  Hivi nyie wanaume hamridhiki na kile Mungu alichowapa?

12/14/2011

Mitihani ya darasa la saba yachakachuliwa wizara husika imetangaza

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Philipo Mulugo akitangaza matokeo ya Mtihani wa Darasa la Saba kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam (Picha na Zacharia Osanga)


WANAFUNZI 9000 WAFUTIWA MATOKEO, HATA WALE WATAKAOINGIA KIDATO CHA KWANZA KUPIMWA UWEZO WAO UPYA 
Gedius Rwiza na Raymond Kaminyoge 
WIZARA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi imetangaza matokeo ya mitihani ya darasa la saba ikieleza kuwa wanafunzi 9000 wamefutiwa matokeo kutokana na udanganyifu na hata wale ambao watapangiwa shule za sekondari wapimwa uwezo wao kabla ya kuanza masomo.  Akitangaza matokeo hayo jijini Dar es Salaam jana, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo pamoja na mambo mengine, alisema kutokana na tatizo hilo, wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza mwakani, watapaswa kuchujwa upya.

“Baada ya udanganyifu kuongezeka mwaka huu,  tumeanzisha utaratibu huu ili kuwabaini wanafunzi wanaingia kidato cha kwanza wakiwa hawajui kuhesabu, kusoma wala kuandika,"alisema Mulugo. 
Mulugo alisema wanafunzi waliofutiwa mtihani huo ni 9,736 na utaratibu wa kuchuja wale waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Kwanza utaanza rasmi Januari mwakani.  Kuhusu wanafunzi kudanganya, alisema Wizara imegundua kuwapo kwa aina nne za udanganyifu ikiwamo wanafunzi 94 kukutwa na majibu katika karatasi, rula na viatu.   

“Watahiniwa wanne walibainika kuandikiwa majibu ambapo ilionekana miandiko zaidi ya mmoja kwenye karatasi ya mtahiniwa  mmoja.  Wataalamu wa masuala ya maandishi wamethibitisha suala hilo,’’alisema Maugo na kutaja udanganyifu mwingine kuwa ni wanafunzi tisa kurudia darasa la saba kinyume na taratibu.  Alisema aina nyingine ya udanganyifu waliougundua ni kuwapo kwa wanafunzi 9,629  waliokuwa na mfanano  usio wa kawaida katika kukosea majibu ya maswali.

Manyara kinara wa kuchakachua
 Waziri Mulugo alisema Mkoa wa Manyara ndio unaoongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya wanafunzi waliofutiwa matokeo. Alisema Mkoa huo una wanafunzi 1, 573 waliofutiwa matokeo, ukifuatiwa na mikoa ya Arusha (1,012) na Lindi (63).  

Akizungumzia kiwango cha ufaulu, Waziri Mulugo, alisema mwaka huu kimeongezeka kwa asilimia 4.76. Kiwango kimepanda hadi asilimia 58.28 kutoka asilimia 53 .52 ya mwaka jana. Mulugo alisema wanafunzi waliofanya mtihani huo walikuwa 983,545 na waliofaulu ni 567,567.  "Wasichana waliofaulu ni  278,377  sawa na asilimia 54.48  na wavulana ni 289,190  sawa na asilimia 62.49," alisema. 

Waziri Mulugo alisema katika kundi la wanafunzi wenye ulemavu, waliofaulu ni 355, kati yao wasichana ni 159 sawa na asilimia 44.79 na wavulana  196 sawa na asilimia 55.21.  Waliochaguliwa  kidato cha kwanza  Waziri Mulugo alisema  kati ya wanafunzi 567,567 waliofaulu,  wanafunzi 515,187 sawa na asilimia 90.1,  wamechaguliwa  kujiunga na kidato cha kwanza katika shule za Serikali huku na 52,380 hawakupata nafasi.  "Wasichana waliochaguliwa ni  253,402 sawa na asilimia 49.1 na wavulana  261,785 sawa na asilimia 50.9," alisema. 

Ufaulu kwa kila somo  Mulugo alisema kuwa viwango vya ufaulu katika masomo ya Kiingereza, Hisabati na Sayansi, vimeongezeka ikilinganishwa na matokeo ya mwaka jana. "Kiwango  cha ufaulu kwa somo la  Kiingereza kimeongezeka kwa asilimia 10.23 kutoka asilimia 36.47 ya mwaka uliopita hadi asilimia 46.70 mwaka huu," alisema.

Naibu Waziri huyo alisema kuwa tofauti na mwaka jana, wahitimu wa mwaka huu wamefanya vizuri katika somo la Hisabati,  hivyo kuongeza kiwango cha ufaulu kutoka asilimia 24.70 hadi asilimia 39.36 mwaka huu.
Alisema katika somo la Sayansi ufaulu umekuwa hadi asilimia 61.33 kutoka asilimia 56.05 mwaka jana. Mulugo alisema viwango vya ufaulu kwa masomo ya Kiswahili na Maarifa ya Jamii vimeporomoka kutoka asilimia 71.02 hadi asilimia 68.58 kwa Kiswahili na kutoka asilimia 68.01 hadi 54.85 kwa Maarifa ya Jamii.
                                               Chanzo ni mwananchi

Mwisho ameamua kufunga ndoa na Merly nchini Namibia.




Wameamua kufanya maamuzi sahihi kufunga ndoa na kuitana mume na mke halali nawatakia maisha mema wao na mtoto wao waliomuita Monkey.

             

12/13/2011

Akamatwa na mihadarati kwenye nywele zake mjini Bangkok siku chache baada ya kuhukumiwa kifo Janice Linden nchini China raia wa Afrika kusini pia.

 


                                   Akiwa anafumuliwa nywele zilizokuwa zimehifadhi madawa

                                            Baada ya kunyolewa nywele zote

NOBANDA NOLUBABALO (23) kutoka Afrika Kusini jana alikamatwa akijaribu kusafirisha madawa ya kulevya aina ya cocaine katika nywele zake za rasta (dreadlocks) katika ndege iliyokuwa inakwenda Bangkok, nchini Thailand.

Nobanda  alikamatwa nchini Thailand na wanausalama waliohisi kulikuwa na kitu cheupe kwenye rasta zake ambapo walipomfanyia upekuzi wakagundua madawa hayo.

Uchunguzi uliofanyika baadaye uligundua kuwa dada huyo alipanda na madawa hayo kabla ya kupanda ndege iliyokuwa inatoka Brazil.

Madawa hayo yanakadiriwa kuwa na thamani ya  Pauni 93,000 ambazo ni sawa na sh. Milioni 235.3 ambapo yeye aliahidiwa kupewa Paundi 1,200 ambazo ni sawa na sh. Milioni tatu.

Kiasi cha kilo 1.5 kiligundulika kwenye rasta za dada huyo.

Nolubabalo bado anashikiliwa na vyombo vya usalama baada ya kukamatwa uwanja wa ndege wa Suvarnabhumi alipotoka katika ndege ya Shirika la Qatar ambayo ilikuwa imetokea Sao Paolo, Brazil, kupitia Doha.

Mwanamke huyo alisema kwamba alikubali kusafirisha madawa hayo baada ya kukubaliana na mfanyabiashara mmoja wa Thailand ambaye angempa Pauni 1,200.

Kukamatwa kwa raia huyo wa Afrika Kusini kunafuatia kunyongwa kwa raia mwingine wa nchi hiyo aliyekamatwa na madawa ya kulevya huko China.

Thailand hutoa adhabu kali dhidi ya wauza madawa ya kulevya ambapo ni pamoja na adhabu ya kifo.

Janice Linden (38) ambaye ni raia wa Afrika Kusini, aliuawa kwa kuchomwa sindano ya sumu jana baada ya kukamatwa katika jiji la Guangzhou, China,  na kilo tatu za madawa kama hayo Novemba 2008.

                                  Marehemu Janice Linden aliyeuawa nchini China kwa sababu ya
                                                          kusafirisha madawa.

12/12/2011

Man city down after accepting 2 strocks from chelsea and the game end 2-1

 
Frank Lampard's late penalty earned Chelsea victory and condemned leaders Manchester City to their first Premier League defeat of the season.
Lampard - once again excluded from Chelsea's starting line-up by manager Andre Villas-Boas - came off the bench to score the winner with seven minutes left after Joleon Lescott handled Daniel Sturridge's shot.
Mario Balotelli gave City a lead their early domination deserved but Chelsea forced their way back into contention through Raul Meireles's equaliser before half-time.
Roberto Mancini's side were reduced to 10 men early in the second half when Gael Clichy was sent off, leaving Chelsea to make the most of their numerical advantage and record a third win in succession to leave City with a two-point lead over neighbours Manchester United at the top of the table.
City will regret not putting the game out of reach in an imperious opening spell - but Chelsea demonstrated the resilience of old to survive that siege and emerge with a win that puts them only seven points off the Premier League summit.
Villas-Boas insisted Chelsea were showing signs of a revival after beating Newcastle United and Valencia following a torrid spell. This, however, was a serious examination of their recovery and they passed the test successfully.
And Lampard, pushed to the margins in the last two games, proved his character to step up under pressure in the closing minutes to convert that vital penalty. Villas-Boas revealed afterwards that Juan Mata had been the designated spot-kick taker, but after a brief discussion with the Spaniard Lampard took responsibility.
City's unbeaten league run came to an end after 15 games - now Mancini and his players must regroup ahead of Sunday's meeting with improving Arsenal at Etihad Stadium.
Chelsea made one enforced change, with Jose Bosingwa replacing the suspended David Luiz - while Balotelli was recalled to instant effect for City.
Manchester City have now had three men sent off in the last six Premier League games
Sergio Aguero must take much of the credit with a turn that left John Terry trailing and a sublime pass with the outside of his right foot into the path of Balotelli. The young Italian may be turbulent elsewhere, but in the penalty area he is calmness personified, as he proved by dismissing the attentions of Branislav Ivanovic to round Petr Cech to score.
City were in command and should have doubled their lead after 14 minutes when Aguero brushed aside Bosingwa and wrong-footed Ashley Cole, only to drag his shot wastefully wide.
David Silva then appealed for a penalty when he fell under Bosingwa's challenge - but referee Mark Clattenburg waved play on while declining to punish the Spaniard for diving.
Chelsea, as much by force of will as any real superiority, dragged themselves into a game which had been completely in City's control and were rewarded with an equaliser 11 minutes before the break. Once again the goal owed almost as much to the creation as the finish, with the impressive Sturridge escaping from the toiling Clichy before crossing for the incoming Meireles to volley powerfully past City keeper Joe Hart.
Former Manchester City player Sturridge was one of Chelsea's leading lights on a stormy evening and he was only just off target with a rising drive a minute after the restart from Mata's free-kick.
City went down to 10 men just before the hour when Clichy, who had been booked early in the second half for fouling Sturridge, tripped Ramires to earn his second yellow card. It capped a miserable night for the defender, who had suffered in the face of Sturridge's pace and threat.
Chelsea, having been outplayed in the early stages, now sensed victory and Villas-Boas introduced Lampard with 17 minutes left in an attempt to make their numbers count.
Mancini appeared to have settled for a point by removing Aguero for Kolo Toure and sending on Nigel de Jong for Silva - but Chelsea were not to be denied.
And Lampard it was who put Chelsea in front with seven minutes left. There were few complaints from City after Sturridge's shot hit the raised hand of Lescott - leaving Lampard to drill the penalty straight down the middle before celebrating with the supporters behind the goal in the Matthew Harding Stand.

Dk. Mwakyembe arejea nchini


NAIBU Waziri wa  Ujenzi na Mbunge wa Kyela, Dk Harrison Mwakyembe, amerejea nchini akitokea Hospitali ya Apollo nchini India alikolazwa kwa ajili ya matibabu ya ugonjwa wa ngozi.  Dk Mwakymbe aliondoka nchini Oktoba 9 mwaka huu kwenda nchini India baada ya hali yake ya afya kuzorota huku ngozi yake ikionekana kudhoofika.

Baada ya kukaa India kwa takriban miezi miwili, jana saa 7:00 mchana, Dk Mwakyembe aliwasili nchini kupitia Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere kwa ndege ya Shirika la Qatar Airways.

Habari zilizolifikia gazeti hili jana mchana zilieleza kuwa baada ya kutua jijini Dar es Salaam, Dk Mwakyembe aliondoka moja kwa moja kuelekea mkoani Mbeya.  Akizungumza na gazeti hili jijini Dar es Salaam jana, Msemaji wa Familia na Mbunge wa Lupa, Victor Mwambalaswa alisema, afya ya mbunge huyo wa Kyela, ni nzuri ndio maana ameruhusiwa kutoka hospitali.

  “Ni kweli Dk Mwakyembe amerejea nchini salama .Tunamshukuru Mungu, hii inatokana na madaktari waliokuwa wakimpatia matibabu kumpa ruhusa baada ya kuona hali yake ni nzuri na kwamba anaweza kuendelea na majukumu yake kama kawaida,” alifafanua Mwambalaswa na kuongeza:

“Kutokana na hali hiyo, tunaamini kuwa, kurudi kwake nchini, kutaleta matumaini mapya ya afya yake.”  Msemaji huyo wa familia alisema, baada ya kurudi, Dk Mwakyembe atapumzika kijijini kwao Kyela ili aweze kujumuika na wanafamilia katika kipindi hiki cha Sikukuu ya Chrismasi na mwaka mpya, kabla ya kuanza kazi rasmi ya ujenzi wa taifa mwakani.

Alisema, kutokana na hali hiyo anaamini, sala za wananchi ni miongoni mwa mambo yaliyofanya apone haraka na kurudi nyumbani Kuugua
Taarifa za kuugua kwa Dk Mwakyembe zilianza kuvuma mwanzoni mwa mwezi Oktoba mwaka huu baada ya kuanza kupata matibabu nchini.

Hata hivyo, kutokana na afya yake kuendelea kuzorota,  Serikali ililazimika kumkimbiza nchini India kwa ajili ya matibabu zaidi.

Taarifa za awali, zilisema Dk Mwakyembe alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kisukari ambapo alikuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Lakini, taarifa hizo za ugonjwa wa kisukari zilipingwa na baadhi ya washirika wake wa karibu kisiasa,  ambao waliamini  Naibu waziri huyo, alilishwa sumu iliyosababisha nywele zake kunyonyoka, ngozi ya mwili wake kupepetuka na kutoa unga, huku akiwa amevimba. Hata hivyio ilielezwa kuwa, madaktari nchini India ndio pekee ambao wangeweza kuangalia namna ya kumsaidia katika ugonjwa huo.