Pages

Sample Text

Frank Kimaro run this blog

11/01/2011

Hali ya Zito kabwe yazidi kuwa mbaya.

Zito Kabwe akia amelazwa hospitalini Muhimbili
(picha kutoka kwenye mtandao)
HALI ya Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) bado ni tete na sasa anapelekwa nchini India kwa matibabu zaidi.
Kwa mujibu wa taarifa ambazo gazeti hili imezipata mchana huu kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili alipokuwa amelazwa, ni kwamba kiongozi huyo ameshauriwa kupelekwa nchini India kwa matibabu zaidi.
Taarifa zaidi zinasema tayari ameelekea katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, na anatarajiwa kuondoka na ndege ya Emirates mchana huu.
“Anapelekwa India kwa matibabu zaidi na huu ni ushauri ambao amepewa na madaktari ambao walikuwa wakimtibu…wanasema anaitaji uangalizi na utulivu wa hali ya juu kimatibabu hivyo wameamua apelekwe nchini India,” alisema kiongozi mmoja wa Chadema akizungumza kwa njia ya simu na mtandao huu.
Mbali na kuzuka kwa taarifa za kutatanisha na za kushtua juu ya hali ya Mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini, jana ililipotiwa kuwa hali yake ni mbaya na amehamishiwa katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU).
Awali Zitto alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Aga Khan, na hali yake ilivyobadilika ghafla jana jioni alipelekwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili. Zitto alilazwa Aga Khan juzi jioni baada ya kusumbuliwa na maumivu ya kichwa kabla ya kuruhusiwa na kisha kurudishwa baada ya maumivu hayo kuendelea.

No comments:

Post a Comment

COMMENT HAPA UKIMALIZA, KWENYE PROFILE SELECT ANONYMOUS KISHA BONYEZA PUBLISH.