Bi Arafa Issa Namaji(Pichani) mwenye umri wa miaka 39 mkazi wa kijiji
cha Narung’ombe wilayani Ruangwa Mkoani Lindi anaomba msaada wa
haraka utakaomuwezesha kupata matibabu ya uvimbe ulio katika paji la
uso uliotokana na maumivu makali ya kichwa baada ya kupata matibabu
katika hospitali ya Ndanda na kuelekezwa kufika katika hospital ya
Taifa ya Muhimbili(MNH) Kwa uchunguzi zaidi na matibabu
Tatizo lilianza tangu mwezi february 2012,alianza kwa kuumwa na
kichwakwa maumivu makali sana na kipele kidogo kikatokea kwenye paji
la uso,hivyo basi kadri kilipopungua maumivu ndipo kipele kiliendelea
kuwa kikubwa hadi kuathiri macho na sehemu ya pua baada ya kuona hali
inazidi kuwa mbaya Majirani na marafiki wa karibu walimshauri kwenda
hospitali ya wilaya,alipofika Daktari alimpa rufaa ya kwenda
hopsitali ya Ndanda,hata hivyo Ndanda pia wakampa rufaa kwenda
hospitali ya rufaa muhimbili kwa uchunguzi zaidi.
kutokana na hali hali hiyo ngumu aliyonayo Kutokana na kuwa katika hali duni na hana mtu yeyote wa kumsaidia Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa wameichangishana kupata
kiasi cha nauli pamoja na hela kidogo ya kujikimu kwa siku
mbili,lakini bado anahitaji msaada zaidi wa pesa kwasababu atahitaji
kuishi zaidi DSM Akiwa katika hospital ya Muhimbili kwa ajili ya
uchunguzi pamoja na matibabu yake
Kwa alietayari kumsaidia anaweza kuwasiliana na Mwenyekiti wa Klabu ya
Waandishi wa Habari mkoa wa Lindi ambae pia ni mwakilishi wa Channel
ten,Abdulaziz Ahmeid kwa namba za simu 0787176221 au 0756696048
Kutoa ni Moyo ili kumsaidia mama huyu
picha na story kwa hisani ya Francis Godwin blogspot
No comments:
Post a Comment
COMMENT HAPA UKIMALIZA, KWENYE PROFILE SELECT ANONYMOUS KISHA BONYEZA PUBLISH.