Na Frank Kimaro
Wafanyakazi wa Tanzania and
Zambia Railway (TAZARA) waliopo kanda maalumu ya Dar es salaam jana walifikia
maamuzi ya kutokufanya kazi mpaka mkurugenzi wa shirika hilo atakapokubali
kuzungumza nao.
Wafanyakazi hao walitoa rai hiyo
baada ya mkurugenzi wa shirika hilo kukataa kuzungumza nao akitoa sababu kwamba
hakuwa tayari mpaka Jumatatu ya wiki ijayo ndipo ataweza kuzungumza juu ya
matakwa yao.
Wafanyakazi hao waliweka bayana
madai mbalimbali ambayo shirika hilo linapaswa kuwatimizia lakini bado mpaka
sasa hayajatimizwa na hakuna sababu za msingi zilizotolewa na kiongozi uongozi mkuu
wa shirika hilo katika kushindwa kutimiza matakwa yao.
“Hatujapata mishahara ya miezi
miwili yani wa 9 na wa 10 na sasa tunaelekea katikati ya mwenzi wa 11, hatuelewi
hatima yetu wakati sisi pia tuna majukumu kama binadamu wengine”Alisikika akisema
mmoja wa wafanyakazi ambaye hakupenda jina lake litajwe.
Mwenyekiti wa Chama cha wafanyakazi
wa reli (TRAWU) kanda maalumu ya Dar es salaam Bw Yusufu Mandai alisema madai yanayotolewa
na wafanyakazi wenzake ni ya msingi na
yanapaswa kutiliwa maanani kwa sababu mshahara ni haki yao ukizingatia
wanafanya kazi.
“Watu wanaishi kutokana na
mishahara inayopatikana hapa si vyema watu kufanya kazi mienzi miwili mfululizo
bila kulipwa mishahara yao,” alisikika akisema.
Msemaji mkuu wa TAZARA, Bw Conrad
Simuchile ameliambia gazeti hili kwamba kwa sasa shirika hilo haliko tayari
kuzungumzia juu ya hali hiyo lakini itatoa tamko siku za karibuni.
“Shirika litatoa kauli kuhusiana
na hali inayoendelea katika siku chache zinazokuja,” alisema Bw Simuchile.
No comments:
Post a Comment
COMMENT HAPA UKIMALIZA, KWENYE PROFILE SELECT ANONYMOUS KISHA BONYEZA PUBLISH.